Haji Manara atangaza kulipa kisasi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 30, 2019

Haji Manara atangaza kulipa kisasi

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara ametangaza kulipa kisasi kwa Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Jumapili hii. 
Haji Manara
Mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro, Simba inazisaka pointi tatu ili kuikimbiza Yanga iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika ujumbe akisema kuwa, "kikosi cha kisasi!. Mbao mtatusamehe kwa kesho, saa mbaya hz!, kipute hiki ni Jumapili ya kesho Jamhuri Stadium Morogoro Saa kumi alasiri".
Katika msimamo wa Ligi Kuu, Simba inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 baada ya kushuka dimbani michezo 21 huku Mbao FC ikiwa katika nafasi ya 14 kwa pointi 36 baada ya kushuka dimbani michezo 30.
Loading...

No comments: