HAWA HAPA MASHUJAA WAMEHUSIKA KUFUZU KWA TANZANIA AFCON 2019, UGANDA BADO WAMO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 24, 2019

HAWA HAPA MASHUJAA WAMEHUSIKA KUFUZU KWA TANZANIA AFCON 2019, UGANDA BADO WAMO

HAWA hapa mashujaa wa leo ambao wamefanikisha timu ya Taifa Stars kuvunja rekodi ya kufuzu Afcon Afrika baada ya miaka 39 kupita Uwanja wa Taifa.

Mashabiki

Kwa nyomi la mashabiki leo haikuwa rahisi kupenya kirahisi kwa Uganda licha ya ubora wao, nguvu ya mashabiki ina nafasi yake, kwa mara ya kwanza ndani ya Uwanja wa Taifa rekodi imewekwa ambapo kabla ya mpira kuanza mashabiki walikuwa wameujaza Uwanja huku wengine wakiwa nje zaidi ya wale walioingia ndani ya Uwanja.

Hamasa ya Serikali

Haikuwa rahisi, Serikali haikuwaacha wachezaji wanyonge kila hatua walikwenda nao bega kwa bega, kamati ya hamasa iliyokuwa chini ya mwenye mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ilikuwa ikizungumza na kutoa hamasa kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa, ile sera ya zima TV tukutane Taifa ikajibu na mwendo wa Zamu Yetu ukatimia.

Wachezaji 

Kila mmoja alikuwa na morali na nguvu ya kupambana ambapo walikula kiapo cha kweli  na kuonyesha thamani ya bendera ya Taifa, hakuna aliyemtegea mwenzake kila mmoja amejitoa kwa moyo wake na kwa nafsi kupambana kufa na kupona kupata matokeo chanya.

Kocha

Ilikuwa ngumu sana kumuuelewa, Emmanuel Ammunike kutokana na mfumo wake ambao anautumia, licha ya kushindwa kueleweka kwa watanzania wengi bado alikuwa na imani kwa kile alichokuwa anakifanya na huenda alipokea ushauri na kufanyia kazi makosa kwenye mechi zake zilizopita hali iliyomfanya leo apate matokeo chanya.

Uwanja

Kuwa nyumbani kumefanya washinde kwani hawakuwa na cha kupoteza leo Uwanja wa Taifa huku nyomi la mashabiki likiwa kama lote hivyo hawakuwa na cha kupoteza Uwanja wa nyumbani.

Kukaza kwa Cape Verde

Dakika 90 za mchezo kati ya Capeverde na Lesotho umekamilika kwa suluhu ya kutofungana hali iliyowafanya Stars kufuzu Afcon.

Msimamo ulivyo kwa sasa

Uganda wanaongoza wakiwa na pointi 13
Tanzania wanafuata wakiwa na pointi 8
Lesotho wanafuata wakiwa na pointi 6
CapeVerde wanafuata wakiwa na pointi 5

Waliozama kambani leo Uwanja wa Taifa ni Simon Msuva dakika ya 21, Erasto Nyoni dakika ya 51 na Agrey Morris dakika ya 57.CHANZO; SALEHE JEMBE
Loading...

No comments: