HEUNG-MIN SON ATUNUKIWA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA KWA TIMU ZA JIJI LA LONDON

Son

Straika wa klabu ya Tottenham Hotspurs, mkorea Heung-Min Son usikuwa kuamkia leo ametunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2019 kwa vilabu vinavyotokea katika jiji la London katika utoaji wa LONDON FOOTBALL AWARDS. 

Mchezaji huyo kutokea nchi ya Korea Kusini, ameibuka kidedea zaidi ya washindane wake wengine kwa kumaliza msimu uliopita akiwa na magoli 16 katika michezo 34 katika michuano yote. 

Son, mwenye miaka 26 pia aliisaidia nchi yake ya Korea Kusini kushinda medali ya Dhahabu katika mashindano ya bara la Asia bila kusahau kuwa amekuwa sehemu muhimu kwa Spurs ambao wanakaribia robo fainali ya logi ya mabingwa barani Ulaya. 

Post a Comment

0 Comments