"HUONDOKI HAPA", CHELSEA WAMCHANA UKWELI HUDSON-ODOI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

"HUONDOKI HAPA", CHELSEA WAMCHANA UKWELI HUDSON-ODOI


Kinda Callum Hudson-Odoi ameambiwa na klabu yake ya Chelsea kwamba hatoondoka klabuni hapo na anapaswa asaini mkataba mpya kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la The Times.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 alishuhudia uhamisho wake wa Pauni Milioni 35 wa kutua Ujerumani kwa klabu ya Bayern Munich ukigonga mwamba mwezi Januari na amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya Stamford Bridge. 

Mkataba wa kijana huyo ndani ya Chelsea unafikia tamati mwaka 2020 na amekuwa kivutio kwa klabu nyingi kubwa barani ulaya.  
Loading...

No comments: