HUU NDIYO UJIO MPYA WA JB - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 30, 2019

HUU NDIYO UJIO MPYA WA JB

Muigizaji na Muandaaji mkongwe wa filamu za kibongo, Jocob Stephen ‘JB’ amewatangazia mashabiki  ujio wa kazi yake mpya itakayokwenda kwa jina la SINGLE MOTHER’S ambayo itazungumzia mengi kuhusu maisha ya wakinamama wanaolea watoto peke yao bila wazazi wenza wao.Kupitia ukurasa wake Instagram JB alianza kwa kumshukuru muigizaji Faiza Ally kwa kumsaidia katika kufanya utafiti juu ya changamoto wanazozipata Single Mother’s.

“Kipekee naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwako @faizaally_ kwa kunikutanisha na group lenu ..group hili ni LA wanawake na wanaumme ambao wanalea watoto peke yao bila wenza wao..ingawa niliomba kukutana na wanawake peke yao...sababu ya project yangu inayokuja SINGLE MOTHER'S..” JB aliandika.

Akilezea alichojifunza kwenye group hilo JB aliandika;

“Nilipata bahati ya kufanya mahojiano nao..ilikuwaje wakachana na wenza wao changamoto..na wanavyojisikia..clip hizo zitakujia hivi karibuni..Lakini pia baadhi yao nimewapa role ndogo..katika tamthilia hii..lililonigusa zaidi ni Wakati nilipounda group LA whats App..daah waliponizoea wakawa wanafunguka..nimejifunza mengi mno.namna wanavyo ishi ..natamani Dunia ingejifunza hivi..usingo mother haujali darasa la saba au PhD.” JB alieleza.

“Lakini kilicho nimaliza wakati nawahoji akatokea mwanaumme ambaye ameachiwa watoto na mkewe..akaniambia jb wasikilize lakini tatizo ni hili ...mjadala mkali ulozuka..ndugu zangu hili ni tatizo kubwa kuliko tunavyo dhani..nusu ya waigizaji toka b..movie ni single moms..mwandishi nae ni single mom..kazi ipo..SINGLE MOTHER'S.. Coming soon”.JB alimaliza.

JB ambaye ni mmilikwa wa kampuni ya utengenezaji wa fialamu ya Jerusalem ni moja kati waigizaji wenye mashabuki wenge kutokata na ubora wa kazi anazozifanya.Masabiki wa filamu za kibongo make mkao wa kula kuisubiri SINGLE MOTHER’S.
Loading...

No comments: