IG kwa ajili ya kuuza au kununua bidhaa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

IG kwa ajili ya kuuza au kununua bidhaaInstagram imekuwa ni sehemu ya watu mbalimbali kujipatia kipato na pengine kama ulikuwa hufahamu kuwa kuna programu tumishi inatengenezwa ambayo itakuwa ni mahususi kwa ajili ya kuuza au kununua bidhaa.

Facebook ambao ndio inayomiliki programu tumishi ya Instagram wameamua kwenda hatua moja mbele kwa kutanua wigo la soko lao ambapo mpaka hivi sasa kuna akaunti za kibiashara Instagram zaidi ya 25 milioni.

Msukumo wa kutengeneza programu tumishi maalum kwa ajili ya wafanyabiashara kuweza kutangaza biashara zao unatokana na wingi wa watu ambao wanathubutu kulipa kiasi fulani cha pesa ili biashara yao iwafikie watu wengi zaidi.

kuuza au kununua
Zaidi ya akaunti za kibiashara 2M wanatangaza biashara zao kwa kulipia ili kile wanachokionyesha kifike mbali zaidi.

Hali iliyo kwenye Instagram.

Watu wanne kati ya watano mmojawapo anafuatilia akaunti ya kibiashara kwenye Instagram na uzuri sio kitu kigumu kabisa kuroka kwenye aina moja hadi nyingine ya akaunti kwenye programu tumisu husika.

Instagram ambao tayari wana IGTV kwa kufanya maamuzi ya kuja na programu tumishi pekee kwa ajili ya wafanyabiashara ni jambo ambalo litatengeneza wigo mpana kati ya mmiliki, muuzaji na mlaji.

Vyanzo: The Verge, Engadget
Loading...

No comments: