JAJI BARNABAS SAMMATA ASHAURI KUBADILISHA JINA LA MAHAKAMA YA MAFISADI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

JAJI BARNABAS SAMMATA ASHAURI KUBADILISHA JINA LA MAHAKAMA YA MAFISADIJaji Mkuu mstaafu na Mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama.
 
*Ahoji kuhusu Mahakama ya mafisadi, ahoji kuhusu jina hilo la Mahakama  mafisadi ni nani katika mahakama hiyo, je ni majaji? Mawakili? Washtakiwa au mashahidi? apendekeza jina hilo kubadilishwa

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
JAJI mkuu mstaafu na Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata ameshauri kubadilishwa kwa jina la mahakama ya mafisadi na litafutwe jina ambalo litasadifu wanaopelekwa katika mahakama hiyo ni washtakiwa.

Akizungumza katika mdahalo uliowakutanisha na wanafunzi wa chuo cha sheria nchini na kujadili mada kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya mahakama jaji Sammata amesema kuwa jina la mahakama ya mafisadi halisadifu wanaopelekwa katika mahakama hiyo kwa kuwa haifamiki mafisadi ni akina nani?, majaji? Mawakili? au mashahidi? na akashauri jina mbadala litafutwe ili kusadifu wanaopelekwa katika mahakama hiyo.

Katika mdahalo huo jaji Sammata alitoa rai kwa wanasheria kote nchini kuwa mstari wa mbele kupinga kansa ya rushwa wakati wa utoaji wa huduma kwa wananchi.
 
Loading...

No comments: