Je unafahamu chanzo cha siku ya Wanawake Duniani ? - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 3, 2019

Je unafahamu chanzo cha siku ya Wanawake Duniani ?

Kila mwaka ifikapo tarehe 8 mwezi machi mataifa mbalimbali duniani huwa yanasherekea siku ya wanawake duniani (International Women's Day). Kauli mbiu ya mwaka huu inasema;
"Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia Kwa Maendeleo Endelevu"


Add caption
Je siku hii ilianzaje?

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Mwaka mmoja baada ya kuanzishwa kwa siku hii maalumu kwa wanawake, chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake. 

Mwanamke aliyejulikana kwa jina Clara Zetkin ndiye alianzisha wazo la siku ya wanawake kuandhimishwa kitaifa. Alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark. Takribani wanawake 100 kutoka nchi 17 walikubaliana kwa pamoja. Kwa mara ya kwanza ilisheherekewa mwaka 1911, Austria, Denmark,Ujerumani na Switzerland.

Suala hilo likawa rasmi mwaka 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuanza kusherehekea siku hiyo na baadae kubuni kauli mbiu ya kwanza mwaka 1996 ilikuwa ''furahia yaliyopita, panga kwa ajili ya baadae''.
Siku ya kimataifa ya wanawake duniani imekuwa siku ya kutathimini maendeleo ya wanawake katika jamii katika nyanja za siasa na uchumi, kulikuwa pia na migomo na maandamano yaliyoratibiwa kwa ajili ya kusisitiza masuala ya usawa.
Moja ya kazi za Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania ni kushirikiana na serikali katika kuhakikisha "Usawa wa Kijinsia" unakuwepo na kumwezesha mwanamke katika kila nyanja. Hivi karibuni mnamo mwaka 2015 Umoja wa Mataifa ulijiwekea malengo 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030 kufikia hayo malengo. Usawa wa Kijinsia ni moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.
Tatizo la ukatili wa kijinsia ni kubwa duniani kote ndio maana Umoja wa Mataifa umelivalia njuga ili kuhakikisha ukatili huo unakomeshwa, lakini pia lengo namba 5 la maendeleo endelevu yaani SDG’s lihusulo "Usawa wa Kijinsia" linatimia ifikapo  2030. Ukosefu wa usawa wa kijinsia unapimwa kila mwaka na ripoti za Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa. Usawa wa kijinsia unafanikishwa kupitia "utendeaji wa haki" kati ya wanaume na wanawake. Wiki ijayo tutakuletea makala ya jinsi watanzania na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na ya kiserikali wanavyosherekea siku ya wanawake duniani. 
Loading...

No comments: