Je wajua unaweza kusafirishwa kwa njia ya Teknolojia kwenda kuwaona Wanyama Serengeti? - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 5, 2019

Je wajua unaweza kusafirishwa kwa njia ya Teknolojia kwenda kuwaona Wanyama Serengeti?Kwenda safari ni ndoto ya watu wengi angalau mara moja katika maisha yao.

Kwa bahati mbaya sio wote wanaoweza kufanya hivyo. Lakini teknolojia mpya ya 'Virtual Reality' nchini Ufaransa inakupa fursa ya kufikia ndoto yako ya kusafirishwa kwa njia ya teknolojia iwezekanavyo.

Wapenzi wa wanyama-pori wanaweza sasa kutazama wanyama wa mwitu katika mabara mengine bila lazima ya kusafiri.

Mradi huu wa 'kuzamishwa' kwenye msitu wa wanyama-pori  ni vyema kuufahamu, kuwa na tabia ya  kupenda wanyama-mwitu na kujisikia karibu nao. Na kuwa karibu nao wakati mwingine unapaswa kwenda Afrika, au kusafiri na kwenda kuwaona katika nchi nyingine, ni vigumu, pia sio  wazo zuri kwa mpango wa muda mrefu. Pia kuna njia nyingine, kama vile zoo, lakini tunadhani kuwa sio ya kuvutia zaidi ya ile ya kwenda mbugani kuona wanyama. Tunataka kutumia teknolojia mpya kwa kusafirishwa kati ya wanyama, "alisema Florent Gilard, msimamizi wa mradi wa "Immersion Wild".

Mradi huo unawapa wageni mtazamo wa wazi, mstari wa mbele wa wanyamapori katika maeneo ya mbali zaidi na ya kigeni, kuwapeleka huko kwa njia ya mchanganyiko wa ukweli halisi na teknolojia ya sauti.

"Tunachotaka kufanya na kivutio hiki ni kuwaonyesha wageni wetu vivutio vya aina yake, kuinua ufahamu wao iwezekanavyo kwa haraka na umuhimu wa kuhifadhi maisha ya wanyamapori," alisema Olivier Bobichon, mkurugenzi wa 'Jardin d'Acclimatation'. 

Teknolojia hii mpya iliyotengenezwa na 'Paris’s oldest theme park' ya Paris inakuja kama ahueni kwa watu wengi wanaoishi Paris yaani Parisians  ingawa wengine wao wanaamini bado haitoshi.
Watengenezaji wa dhana hii wanapanga kuhusisha hisia kwenye hii teknolojia ya 'VR' kama vile harufu na kugusa kupitia timu ya ubunifu. 
Kusoma Zaidi Makala hii tembelea tovuti ya AfricanNews
Loading...

No comments: