JENNIFFER HUDSON KUCHEZA UHUSIKA WA MAREHEMU ARETHA FRANKLIN KWENYE FILAMU MPYA YA MAISHA YAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 12, 2019

JENNIFFER HUDSON KUCHEZA UHUSIKA WA MAREHEMU ARETHA FRANKLIN KWENYE FILAMU MPYA YA MAISHA YAKE


Malkia wa muziki wa Soul na R&B Aretha Franklin hatuna naye tena. Sasa kinachofuata ni filamu fupi ya maisha yake ambayo imepewa jina la 'Respect' na imetajwa kutoka August 2020 chini ya kampuni ya MGM.

Nyota ambaye ametajwa kuvaa uhusika wa marehemu Aretha Franklin ni mwimbaji Jennifer Hudson. Jarida la Deadline limeeleza kuwa filamu hiyo itagusa maisha yake kuanzia utoto, kuanza kuimba kwenye kwaya ya Baba yake ambaye alikuwa mchungaji hadi kuingia rasmi kwenye muziki na kuwa maarufu.

Aretha Franklin alifariki dunia August 2018 akiwa na umri wa miaka 76 mara baada ya kupambana kwa muda mrefu na ugonjwa wa saratani ya kongosho.
Loading...

No comments: