Jerry Muro Azungumzia Kumng'oa Mbowe 2020 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 26, 2019

Jerry Muro Azungumzia Kumng'oa Mbowe 2020

Akiongea kwenye kipindi cha East Africa Break Fast cha East Africa Radio, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amezungumzia mpango wake wa kuwania Ubunge katika jimbo la Hai kweye Uchaguzi Mkuu 2020, ambalo kwa sasa linaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe ambapo amesema suala hilo linahitaji neema za Mungu.


Jerry Muro amesema ni kweli kumekuwa na maneno ya watu wengi wanaodai kuwa anaonekana mara kwa mara akifanya harambee kwenye jimbo la Hai.

Swali
Mtangazaji Charles William, "ukiwa jijini Dar es salaam ulionekana ukijitambulisha kama mkazi wa Ubungo Maziwa na mara kwa mara ulionekana ukimkosoa Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea, na sasa unaonekaa umelenga kuingia jimbo la Hai ni kweli unalitaka jimbo lile"? 

Majibu

 Jerry Muro, "hakuna binadamu anayeishi bila matamanio, mimi siwezi kusema matamanio yangu ni nini lakini Mungu akisema uwe Mbunge utakuwa lakini akisema usiwe Mbunge hata ufanye harambee 500 hutakuwa Mbunge, niwaambie watanzania masuala ya Ubunge yanahitaji kumtazama Mungu".

"Wanaokwambia Jerry Muro anataka Ubunge ujue wanamatamanio mimi niwe Mbunge wao, kwa hiyo kama wewe unajua mwambie Mbowe ikiwaka mulika, ikizimika papasa".ameongeza Jerry Muro.

 Mwaka ujao, 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu hapa nchini Tanzanzania, hivyo kwasasa wanasiasa wengi wameshaanza kuonyesha nia ya kugombea kwenye majimbo mbali mbali.

Loading...

No comments: