JOHARI: SIWEZI KUOLEWA NA MUIGIZAJI MWENZANGU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 25, 2019

JOHARI: SIWEZI KUOLEWA NA MUIGIZAJI MWENZANGU

Msanii mkongwe na mrembo kutoka kiwanda cha Bongo movie, Blandina Chagula ‘Johari’, amefunguka kuwa hafikirii kuolewa na muingizaji mwenzake mwenzake sababu ya changamoto zilizopo kwenye kazi hiyo.

Blandina Chagula ‘Johari’

Akiongea na gazeti la Dimba hivi karibunu, Johari, ambaye ni mama wa mtoto moja aitwaye Maria, alifunguka kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mtu ambaye sio masanii na hataki kuyaweka wazi mahusiano yake.

 “Watu walizungumza mengi, wengine wakifikiria natembea na msanii mwenzangu, Ray Kigosi, kitu ambacho si kweli na wengine walidiriki kudai nina mtoto wake, nataka watambue kuwa sifikirii kuingia kwenye maisha ya ndoa na msanii wala kwa sasa sipo na mtu ambaye ni msanii". alisema Johari aliliambia gazeti hilo.

Akizungumzia kuhusu kumuingiza mtoto wake kwenye tasnia ya filamu Johari alifunguka;

 “Siwezi kumuingiza mwanangu katika kuigiza maana huwezi kufahamu kipaji cha mtu akiwa bado mdogo maana ndio kwanza ana miaka mitatu". 


Johari na msanii mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray Kigosi’ ni wakurugezi wa kampuni yao ya RJ Company inayojishughulisha na utengenezaji wa filamu.
Loading...

No comments: