JORDI ALBA ASAINI MKATABA MPYA NA FC BARCELONA MPAKA 2024 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

JORDI ALBA ASAINI MKATABA MPYA NA FC BARCELONA MPAKA 2024

Alba

Beki wa kushoto wa klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania, Jordi Alba amesaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Camp Nou na kuitumikia timu hiyo mpaka mnamo mwaka 2024. 

Mkataba huo mpya wa Alba mwenye umri wa miaka 29 una kipengele cha thamani yake ya Euro Milioni 500 (Buy-Out Clause) .

Jordi amekuwa na uhusiano na uelewano mzuri na mshambuliaji na nyota wa klabu hiyo Lionel Messi na kusababisha magoli mengi kutokea upande wa kushoto anapocheza Alba. 

Jordi Alba (kushoto) akifurahia ushundi na nahodha wa Fc Barcelona, Lionel Messi
Alba alijiunga na Barcelona kutoka klabu ya Valencia mwaka 2012 na amefanikiwa kucheza mechi 282, kutwaa mataji 14 na katika hayo manne kuna mataji manne ya ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga. 


Loading...

No comments: