JUVENTUS WAANZA KUMNYEMELEA KANTE, WAPO TAYARI KUSHINDANA NA REAL MADRID - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 21, 2019

JUVENTUS WAANZA KUMNYEMELEA KANTE, WAPO TAYARI KUSHINDANA NA REAL MADRID


Klabu ya Juventus ya Italia imeripotiwa kujiunga kwenye mchakato mkali na Real Madrid ya Hispania wa kuwania kupata saini ya kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante katika majira ya kiangazi. 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Le 10 Sport, mabingwa hao watetezi wa Serie A wapo tayari kuingia vitani dhidi ya Real Madrid kwa Mfaransa huyo mapema tu pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa. 

Wakati huo huo mabingwa wa Ufaransa PSG nao wameripotiwa na Le 10 Sport kwamba wanafuatilia kwa ukaribu hali ya Kante ndani ya klabu ya Chelsea ambapo imeripotiwa kuwa hafurahishwi na nafasi anayochezeshwa uwanjani na kocha Maurizio Sarri, kutoka kuwa kiungo Mkabaji mpaka kuwa kiungo mshambuliaji. 
Loading...

No comments: