Kagere ashinda tuzo, tetesi za kutua Misri zaibuka - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 6, 2019

Kagere ashinda tuzo, tetesi za kutua Misri zaibuka


Mshambuliaji wa timu ya Simba, Meddie Kagere amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL). 
Meddie Kagere.
Kagere raia wa Rwanda ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salim Aiyee wa Mwadui na Salum Kimenya wa Prisons alioingia nao fainali.
Mbali na kushinda tuzo hiyo, ripoti kutoka nchini Misri zinaeleza kuwa nyota huyo ambaye ni kinara wa mabao wa Simba msimu huu, anawindwa na klabu ya Zamalek SC ya Misri.
Imeelezwa kuwa Zamalek SC ipo tayari kulipa kiasi cha dola 450,000 zaidi ya shilingi Bilioni 1, kwaajili ya kupaa saini ya Kagere ambaye yupo nchini Algeria na kikosi cha Simba ambacho kitakipiga na JS Saoura ya huko Jumamosi hii.
Timu za Misri zimekuwa zikiwinda wachezaji kutoka ligi kuu soka Tanzania, ambapo tayari zimeshawanasa Himid Mao na Shiza Kichuya wakati Obrey Chirwa aliondoka Yanga akatimkia Misri kabla ya kurejea Azam FC.
Loading...

No comments: