KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 6, 2019

KAMATI YA BUNGE YATAKA MFUKO WA TAIFA WA UKIMWI KUJITEGEMEA.

Na Mwandishi wetu

Serikali imetakiwa kutenga bajeti ya kutosheleza ili kuuwezesha Mfuko wa Taifa wa Ukimwi kujitegemea na kuepukana na utegemezi wa fedha za wafadhili katika mapambano ya Virusi vya Ukimwi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI na Madawa ya kulevya  Oscar Mukasa wakati wa kamati hiyo ilipofanya ziara  katika Kitengo cha kutolea dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (CTC) katika Hospitali ya Wilaya ya Ubungo kujionea hali ya utoaji huduma.

Mhe. Oscar Mukasa (MB) amesema suala la upatikanaji wa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ni jambo la kitaifa na kamati yake ina mkakati wa kuhakikisha inaongeza nguvu kwenye Mfuko wa Taifa wa Ukimwi (ATF) na nchi kuweza kujitegemea kuhusu masuala ya  UKIMWI.


Wajumbe wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madawa wakimsikiliza mtoa huduma za afya katika Kituo cha kutolea dawa za kufubaza Virusi vyta Ukimwi (CTC) katika Hospitali ya Sinza.

Tuna haja ya kujipanga wenyewe kuhakikisha kwamba tunajitegemea, ule utegemezi wa fedha za wadau za mapambano ya Ukimwi unaweza kupungua”. amesema Mhe. Mukasa.

Mhe. Mukasa amesema Serikali imekuwa ikitegemea fedha za wafadhili kutoka nje ya nchi na sasa ni vizuri tukajipanga wenyewe na kuacha utegemezi wa wafadhili hao kutoa fedha muda wote.

Hata hivyo Mhe. Mukasa amesema kamati yake itaendelea kusimamia Serikali hasa Wizara ya fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha  wanapata chanzo mahsusi cha kodi kwa ajili ya ATF.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo na pia Waziri mwenye dhamana ya Afya, Maendeleo ye Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amefurahishwa kuona Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeanza kutekeleza agizo alilolitoa la kutoa ushauri, kupima pamoja na matibabu ya kufubaza virusi vya ukimwi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Masuala ya UKIMWI na Madwa ya Kulevya, Mhe. Oscar Mukasa akisema jambo kwa wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) katika ziara ya wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea Mkoa wa Dar Es Salaam kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya kwenye matibau ya Virusi vya Ukimwi

Aidha, Waziri Ummy ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kutekeleza agizo la Serikali kwa kutoa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi kwa muda kwa kipindi cha miezi mitatu kwa wagonjwa ambao wameshachunguzwa na kubainika virusi kufubaa.

“Mpango wetu Serikali kwa wagonjwa ambao watakao kidhi vigezo basi watazipate dawa hizo kwa miezi sita”.  Alisema Waziri Ummy na kuendelea kuwa wanalenga kuwaondolea usumbufu wa kuja mara kwa mara.


Loading...

No comments: