KARDINALI AHUKUMIWA KWA KUSHINDWA KUKEMEA UNYANYASAJI DHIDI YA WATOTO


Kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Ufaransa, Kardinali Philippe Barbarin amehukumiwa jana Alhamisi Machi 7 na Mahakama ya Jinai ya Lyon kifungo cha miezi sita jela.

Mahakama imempata na hatia ya kushindwa kukemea na kukaa kimya kwa vitendo udhalilisha dhidi ya watoto kwa kasisi wa dayosisi yake. Saa chache baada ya uamuzi huo wa mahakama, Kardinali Barbarin ametangaza kwamba anatarajia kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa Papa Francis.

Mahakama ya Ufaransa imempata na hatia kiongozi wa ngazi ya juu katika kanisa nchini humo na kumhukumu kifungo cha miezi dita jela. Wakati wa hukumu hiyo, huyoKardinali Barbarin hakuwepo.

Jaji mkuu wa Mahakama ya Jinai ya Lyon, Brigitte Verney, amempata na hatia ya kushindwa kukemea kitendo kichafudhidi ya mtoto mmoja kati ya mwaka 2014 na 2015.

Wanasheria wa Kardinali Barbarin wametangaza kuwa watakata rufaa. "Hoja ya mahakama haiiniingia akilini. Kwa hiyo tutapinga uamuzi huu kwa njia zote muhimu za kisheria" amesema Jean-Felix Luciani, akibainisha kuwa ilikuwa vigumu kwa mahakama kukataa shinikizo hilo. 

CHANZO: RFI

Post a Comment

0 Comments