KATIKA HARAKATI ZA KUTAFUTA STRAIKA MWINGINE, SUAREZ AMPENDEKEZA MAX GOMEZ KWA LIVERPOOL - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

KATIKA HARAKATI ZA KUTAFUTA STRAIKA MWINGINE, SUAREZ AMPENDEKEZA MAX GOMEZ KWA LIVERPOOL


Imeripotiwa kuwa klabu ya Liverpool wanamtaka Straika wa klabu ya Celta Vigo, Maxi Gomez mwenye thamani ya Pauni Milioni 35 baada ya kushauriwa na straika wao wa zamani Luis Suarez. 

Gomez mwenye umri wa miaka 22, ni straika wa kimataifa wa Uruguay na amefanikiwa kucheza mechi 9 za kimataifa. 

Gomez yupo kwenye kiwango kizuri sana kwani anakaribia kufikisha rekodi ya kufunga magoli 10+ katika misimu miwili mfululizo kwani Msimu uliopita alifunga magoli 17 na msimu huu tayari ana magoli 9 katika ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama LALIGA. 
Loading...

No comments: