KILIMO CHA KIDIGITALI - E-KILIMO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 31, 2019

KILIMO CHA KIDIGITALI - E-KILIMO

Fursa kwa vijana ni wajibu wetu sisi wanahabari kukupa taarifa za fursa mbalimbali, hakuna sababu tena ya kulalamika kuwa huna taarifa, sasa ni wewe tu ushindwe kuzichukua na kuzifanyia kazi.

Je wafahamu kuhusu nini e-kilimo Accelerator? 

Ni programu ya teknolojia kwenye kilimo na inayowezesha wadau mbali mbali wa kilimo kuanzisha biashara au kuendeleza biashara ya kilimo. 


E-Kilimo ni program yenye nia ya kuanzisha kasi ya juu ya vifaa vya digitali na maendeleo ya teknolojia ili kuharakisha ukuaji wa mawazo na kuanzisha biashara ambayo inaweza kuleta matokeo chanya katika sekta ya chakula na kilimo. Programu hii ina lengo la kusaidia mawazo kaitika hatua za awali na mawazo mapya ya kibiashara katika sekta ya kilimo kupitia ushauri, msaada wa kiufundi, fedha, na mbegu.

Je una wazo la kibiashara kwenye maeneo haya?

1. Precision Farming and Automation Technologies.

Teknolojia zinazoongeza ufanisi wa kilimo na ufanisi wa; Drones, Umwagiliaji wa kutumia drip (matone), Agri Solutions, Sensors Smart na 3D Printing. Kipaumbele kitapewa kwa suluhisho zinazozalisha taarifa, vifaa vya kuunganisha (Internet of Things) na mifumo ya kidigitali ya kutumia roboti.

2. Teknolojia ya Agri-Fintech na Biashara ya kidigitali.

Teknolojia zinazohamasisha wakulima kwenye ujuzi na uelewa wa kifedha na huwapa fursa ya kufanya biashara kwa ujuzi; mifumo ya kupata mikopo, mifumo ya biashara na kubadilishana, upatikanaji wa mikopo, usimamizi wa makundi ya akiba na akaunti za pamoja.

3. Agrotech Systems ya Kuimarisha Usalama na Uzalishaji.

Mifumo ya kutoa taarifa; teknolojia zinazowaonya wakulima juu ya majanga mapya kwa mfano aina mpya za wadudu zinazoathiri mazao yake. Usimamizi wa mnyororo wa ugavi, teknolojia zinazoboresha changamoto za vifaa kwa mkulima na rasilimali zilizounganishwa  kwa mfano utumiaji wa uber kwa matrekta nk.


4. Kilimo cha mjini na na Teknolojia ya baada ya  Mavuno.  
Suluhisho la uhifadhi na ufungaji ambao husaidia wakulima kusimamia mazao yao ya kilimo baada ya mchakato wa kuvuna. Pia, mbinu mpya za ubunifu za kilimo cha mijini huchukua teknolojia na digitali katika mchakato.

Kupata taarifa zaidi tembelea E-Kilimo Accelerator


Loading...

No comments: