KISA MABAO YA STARS, DIAMOND & ZARI WARUSHIANA MANENO MAZITO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 26, 2019

KISA MABAO YA STARS, DIAMOND & ZARI WARUSHIANA MANENO MAZITO
STAA wa Bongo Flva, Diamond Platnumz na mzazi mwenzake Zari the Boss Lady wameingia tena kwenye vita nzito baada ya kurushiana maneno katika akaunti zao za instagram kufuatia ushindi wa bao 3-0, kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Uganda, jana Jumapili, Machi 24, 2019.

Diamond ndiye alikuwa wa kwanza kwa ku-post maneno ya kuishabikia Stars huku akiweka utani wa kichokozi kwa Waganda baada ya bao la kwanza la Simon Msuva, kwa kuandika, “Najua mpira haujaisha ila nawajuza tu wajomba zake kina Tiffah hapo mji Kampala….”

Kwa hiyo post ya kwanza Zari alinyamaza hakutoa neno lolote lakini baada ya mechi kumalizika Diamond ali-post kipande cha video cha wachezaji wa Stars wakishangilia na kuandika, “Kama tuliwafunga magoli ya watoto, tutashindwa ya mpira…..Ebu watagi waganda wote chini waambie Simba kasema ‘TETEMA'”

Kwa upande wa mzazi mwenzake ambaye ni Zari naye akaamua kujibu mapigo baada ya kuweka post iliyokuwa inaonyesha msimamo wa matokeo ya Kundi L ambapo Uganda na Stars wamefuzu; “Nisaidie kutag ma bogus wote tell them we already qualified for the African cup of nations.Manenos yakue madogo,VIVA UGANDA”.
Loading...

No comments: