KISUTU: MKURUGENZI WA M HOLDINGS GROUP INAYOMILIKI BANK M AFIKISHWA MAHAKAMANI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 7, 2019

KISUTU: MKURUGENZI WA M HOLDINGS GROUP INAYOMILIKI BANK M AFIKISHWA MAHAKAMANI


Habari zilizotufikia muda huu zinabainisha kuwa aliyekuwa Mkurugenzi Bank M na CEO wa M Holdings Group, SANJEEV KUMAR, amekamatwa na Vyombo vya Dola na leo amefikishwa mahakamani Kisutu.

KUMAR amefikishwa mbele ya Hakimu Huruma Shaidi na anasomewa mashtaka yanayomkabili ikiwemo ya utakatishaji fedha. 

Sanjeev Kumar amesomewa Mashtaka yenye Makosa 29 yakiwemo 12 ya kutakatisha fedha na amekosa dhamana na hivyo kwenda mahabusu moja kwa moja. 

Ikumbukwe kuwa siku si nyingi Bank M imechukuliwa na benki ya Azania kwa sasa mara baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya BOT. 

No comments: