Kiwanda cha mabehewa kujengwa Tanzania - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

Kiwanda cha mabehewa kujengwa Tanzania

Dhamira ya serikali ya awmu ya tano ya kuinua uchumi kupitia sekta ya viwanda inazidi kupata nguvu na kuungwa mkono na wawekezaji wa ndani na nje, ambapo mwekezaji mzawa ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya kiluwa group, Mohammed Kiluwa ametangaza dhamira ya kuwekeza katika miundombinu ya usafirishaji kwa kujenga kiwanda cha mabehewa kwa ajili ya reli za kisasa na zamani.

Akiwa katika hafla ya kubadilishana nyaraka za makubaliano aliyoingia na kampuni ya Afrika jambo group ya Afrika kusini jijini Johannesburg hivi karibuni, Kiiluwa alisema anataka kufanya kitu cha kipekee katika ardhi ya Tanzania kwa faida ya Nchi na mataifa mengi barani Afrika.

Kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la uwekezaji Kiluwa Free Processing Zone mkoani pwani na kitagharimu doll za Marekani milioni 150 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo ambao unatarajiwa utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda Nchini pamoja na usafirishaji. Utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa awamu tatu huku kila awamu ikiajiri watu 980.
Loading...

No comments: