KOCHA WA LYON: "NITAJISIKIA HESHIMA SANA KAMA MOURINHO AKIWA MRITHI WANGU" - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

KOCHA WA LYON: "NITAJISIKIA HESHIMA SANA KAMA MOURINHO AKIWA MRITHI WANGU"


Kocha wa klabu ya Olympique Lyon, Bruno Genesio, amesema kwamba atajisikia heshima sana kama mrithi wake atakuwa ni mreno Jose Mourinho. 

"Tunachoweza kufanya ni kumheshimu Mourinho. Ameshinda kila sehemu alipoenda. Namuheshimu sana na rekodi yake na yale mataji aliyotwaa."

"Kila alipoenda ametwaa mataji, amewahi kutwaa taji la UEFA kwahiyo kama akija kuwa mrithi wangu itakuwa heshima kubwa sana kwangu"

Je Mourinho atatua Lyon?
Loading...

No comments: