KUMEKUCHA!! KAPOMBE AREJEA RASMI KAZINI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 24, 2019

KUMEKUCHA!! KAPOMBE AREJEA RASMI KAZINI


BAADA ya kuwa nje tangu Novemba mwaka jana, beki wa Simba, Shomary Kapombe sasa yuko fi ti na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi wiki ijayo.

Kapombe aliumia kifundo cha mguu kwenye kambi ya Taifa Stars iliyowekwa nchini Afrika Kusini ambako walikuwa wakijiandaa na mechi dhidi ya Lesotho, beki huyo alifanyiwa upasuaji.

Kwa mujibu wa Championi Jumamosi, Kapombe alisema amefanyiwa vipimo na wamebaini kwa sasa yupo vizuri na ameanza mazoezi mepesi.

“Nilienda Afrika Kusini kufanyiwa vipimo ili kujua maendeleo yangu yako vipi, kwa sasa vipimo vinaonyesha nipo vizuri na nimerejea nchini na sasa kuwa mazuri nitaungana na timu kuanza mazoezi lakini kwa sasa namshukuru Mungu niko fi ti kiafya,” alisema Kapombe.
Loading...

No comments: