Kutazama Televisheni na Vifaa Vingine vya Kielektroniki Hupunguza Uwezo wa Akili wa Watoto! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 3, 2019

Kutazama Televisheni na Vifaa Vingine vya Kielektroniki Hupunguza Uwezo wa Akili wa Watoto!

Utafiti uliochapwa kwenye jarida la Lancet, ulihusisha watoto 4,524 wenye umri wa miaka 8 hadi 11 waliofanya majaribio 6 yanayopima uwezo wa lugha, kumbukumbu, uwezo wa kupanga & kasi ya kumaliza majaribio ya akili.


Ikilinganishwa na watoto waliokuwa hawafuati vigezo vya mazoezi, usingizi na muda wa kuangalia televisheni, watoto waliofuata vigezo walipata 4% zaidi kwenye majaribio kuliko wengine. 30% ya watoto waliofanyiwa utafiti hawakukidhi mapendekezo hayo matatu.


"Muda unaotumia kuangalia televisheni au vifaa vya kielektroniki unaathiri usingizi" alisema Jeremy J. Walsh, kiongozi wa utafiti kutoka Chuo Kikuu cha British Columbia. "Kulala usingizi ni tabia muhimu kwa kuunda vizuri ubongo. Watoto wanahitaji kusinzia masaa 9 hadi 11 wakati wa usiku ili kufanya ukuaji wao kiakili inavyotakiwa" aliongezea.Angalau dakika 60 za mazoezi, masaaa 9 hadi 11 ya usingizi wa usiku na kuangalia televisheni chini ya masaaa mawili, mapendekezo haya matatu yanahusishwa na ufaulu mzuri kwenye majaribio ya akili. Kucheza, kuimba na kuwasomea hadithi nzuri watoto wa kati ya miaka miwili na minne husaidia ubongo wa watoto kukua vizuri.

No comments: