Kuwa sehemu salama dhidi ya wadukuzi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 7, 2019

Kuwa sehemu salama dhidi ya wadukuzi


Udukuzi ni suala ambalo linasumbua mataifa mengi duniani na kila leo yanapambana dhidi ya wale ambao wanapenda kuchungulia vitu vya watu bila ridhaa kitu ambacho kimezalisha mbinu za kuwa salama dhidi ya wadukuzi.

Elimu dhidi ya udukuzi kwa maana ya kwamba ukitaka kujua jinsi ya kuwa mdukuzi inaweza ikawa ni kero kwa mhusika hasa iwapo hana chembe ya ujuzi kuhusu uandishi wa programu, masuala ya intaneti, n.k lakini kitu kizuri ni kwamba sio lazima wote tuwe wadukuzi ndio tujue jinsi ya kujilinda. Unaweza kutumia njia zifuatazo kujihami dhidi ya udukuzi:-

Tengeneza nenosiri gumu.

Moja ya njia nyepesi kwa wadukuzi kufanikiwa kuingia kwenye akaunti ya mtu inasababishwa na mtu kutumia nywila ambayo ni rahisi kufikirika mathalani unapoamua kutumia mwaka wa kulizaliwa jina la mke au mtoto, tarakimu 1234, n.k. Hivyo basi, unatakiwa kutengeneza nenosiri ambayo kamwe itakuwa ni vigunmu mtu kuotea.
salama dhidi ya wadukuzi
Mfano wa nenosiri ambayo ni ngumu mtu mwingine kuiotea.

Nywila ni siri yako mwenyewe.

Kwa sababu moja au nyingine unaweza ukaamua kumwambia mtu nenosiri unayotumia kwenye akaunti fulani lakini daima inashauriwa kutomwambia mtu yeyote nywila hii ikijumuisha hata zile unazotumia kwenye simu, tabiti, kompyuta.
salama dhidi ya wadukuzi

Nywila ni siri yako mwenyewe.

Badilisha nenosiri kila baada ya muda fulani.

Wengi wetu tumekuwa na tabia ya kutumia nywila moja kwa muda mrefu, nikupe ushauri wa bure tuu kwamba mazoea hayo ni mabaya kabisa kwani unawapa mwaya wadukuzi kuweza kuijua na hatimae kuweza kutekeleza kile wanachokihitaji kwenye akaunti yako.
Ni vyema ukabadilisha nenosiri kila badda ya miezi 3-6, usitumie nywila sawa kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, n.k).
salama dhidi ya wadukuzi
Ukibadilisha nywila usibadilishe herufi/tarakimu moja bali badilisha mchanganyiko mzima wa nenosiri.

Njia mbili za kuidhisha kuingia kwenye akaunti.

Moja ya njia ya kufanya udukuzi kuwa na changamoto ni kutumia njia mbili ambazo zitahitajika kuruhusu mtu kuingia kwenye kwenye akaunti; hii inamaanisha kuingiza tarakimu maalum ambazo zitatumwa kwenye namba yako ya simu na kuziingiza kwenye akaunti husika.
salama dhidi ya wadukuzi

Ukitumia “Two-step verification” maana yake ni mbali na kuweka nywila itakulazimu kuweka tarakimu ambazo zitakuwa zinatumwa kwenye namba yako na kamwe hazitowahi kufanana.

Soma kwa umakini sera ya faragha kwenye mtandao/tovuti husika.

Wengi wetu huwa hatuna tabia ya kuchukua muda kidogo kusoma na kuelewa ni namna gani ambayo mtandao/tovuti itakuwa ikitumia taarifa zangu binafsi kwa Kiingereza tunasema “Privacy Policy“. Ni muhimu sana kuelewa kipengele hiki pale unapotaka kujiunga kwenye mtandao wa kijamii au sehemu nyingine ambayo itahitaji weke taarifa zako binafsi.
salama dhidi ya wadukuzi
Mfano wa sera ya taarifa binafsi za watu kwenye tovuti fulani.

Tembelea tovuti ambayo ni salama.

Moja ya njia ambayo unaweza kuwa na uhakika kuwa sio tovuti ya kutia shaka ni pale unapoona inatumia “https” au alama ya kufuli kabla ya utambulisho wa tovuti husika. Kama utakuta tovuti haina vitu hivyo viwili basi itakubidi uwe mwangalifu sana kuhusu taarifa unazoweka kwenye mtandao huo.

Kwanini utembelee tovuti salama tu?

Tovuti ambazo zina alama ya kufuli/https zinakuwa na ulinzi wa aina fulani ambao unazikinga kuingiliwa kirahisi na wadukuzi lakini pia mtu makini anaetunza tovuti anakuwa mfuatiliaji wa mara kwa mara hivyo kuchuja/kuondoa vimelea vyote ambayo amevitilia shaka.
salama dhidi ya wadukuzi
Moja ya tovuti salama.

Kumbuka kufunga akakunti yako baada ya kumaliza kutumia.

Ni lazima ufikirie kila namna ambayo itakuwa ni ngumu kwa mdukuzi kuingia kwenye akaunti yako na moja ya njia rahisi kabisa ni kutoka kabisa mara tu utakapomaliza shida zako.
salama dhidi ya wadukuzi
Hii inasaidia pale mtu atakapoamua kutembelea tovuti husika kupitia kifaa chako kwahiyo kufunga tuu kivinjari haitoshi bali inakupasa kutoka kabisa.

Njia za kufanya akaunti iwe salama zipo nyingi lakini daima tunapenda kuleta machoni pa watu mbinu ambazo hazitakuwa na changamoto kutokana na sababu mbalimbali.

Loading...

No comments: