LEBRON JAMES AVUNJIKA MOYO BAADA YA LAKERS KUPOKEA KICHAPO CHA 3 MFULULIZO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 5, 2019

LEBRON JAMES AVUNJIKA MOYO BAADA YA LAKERS KUPOKEA KICHAPO CHA 3 MFULULIZOYale matumaini ya mchezaji maarufu wa kikapu ulimwenguni LEBRON JAMES ya kuweza kuifanikisha timu yake ya Los Angeles LAKERS kufikia japo hatua ya mtoano katika msimu yameanza kuyeyuka mara baada ya jana kupokea kichapo cha tatu mfululizo tokea arejee kutoka maumivu. 


LAKERS wamepokea kichapo hicho kutoka kwa timu ya LA CLIPPERS ambayo wanatoka nayo mji mmoja kwa vikapu 113-105. 

Mchezaji Danielo Gallinari wa LA CLIPPERS alionekana kung'aa sana katika mchezo huo uliokuwa wa muhimu kwa kila timu na alimaliza mchezo akiwa na pointi 23 na kuisaidia timu yake kufikia nafasi ya 7 katika msimamo wa kanda ya Magharibi. 

Pamoja na Lebron James kufunga pointi 27, rebound 8 na assist 6, bado haikutosha kuwashinda CLIPPERS ambao walikuwa nyumbani kwao na walionyesha njaa kubwa sana ya kutaka kushinda mchezo huo huku wakiwa vizuri kwenye eneo la ulinzi kwa quarter 3 za mwanzo. LAKERS kwa sasa wapo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi hiyo kwa kanda ya Magharibi. 


Nafasi hiyo waliyopo haiwapi uhakika wa kucheza hatua ya mtoano kwani zinahitajika timu 8 kutoka katika kila kanda na wao wapo nafasi ya 10. 

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA: 

  • Los Angeles Clippers 113-105 Los Angeles Lakers
  • Milwaukee Bucks 105-114 Phoenix Suns
  • New Orleans Pelicans 115-112 Utah Jazz
  • Denver Nuggets 103-104 San Antonio Spurs
  • Atlanta Hawks 113-114 Miami Heat
  • New York Knicks 108-115 Sacramento Kings
  • Dallas Mavericks 88-127 Brooklyn Nets
Loading...

No comments: