LEO NDIO LEO USIKU WA ULAYA, JE AJAX ATAMALIZA UTEJA KWA MADRID? DORTMUND NDIO KWAHERI? - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 5, 2019

LEO NDIO LEO USIKU WA ULAYA, JE AJAX ATAMALIZA UTEJA KWA MADRID? DORTMUND NDIO KWAHERI?


Ligi ya mabingwa barani ulaya imerejea tena na leo jumanne kuna mechi kali 2. Borussia Dortmund watawakaribisha Tottenham Hotspurs, na Real Madrid watawakaribisha Ajax Amsterdam pale Santiago Bernabeu. 

Hizi ni mechi za raundi ya mtoano na leo ni marudiano tu na matokeo ya mechi za leo ndio yataamua nani aingie hatua ya robo fainali. 

Katika raundi ya kwanza, Real madrid walipata ushindi wa 2-1 ugenini, huku Borussia Dortmund iliyokuwa katika fomu nzuri sana ilichabangwa 3-0 na Spurs pale Wembley ambao ndio uwanja wa nyumbani wa Tottenham. 


Leo, Dortmund wapo nyumbani lakini fomu yao haipo vizuri kabisa. wamekuwa watu wa kupoteza michezo na kutoa droo nyingi tofauti na mwanzo wa msimu walivyokuwa. Mechi yao ya jumamosi walichapwa 2-1 na Augsburg na wanaandamwa na majeruhi kama ya Paco Alcacer pamoja na Marco Reus ambao ni wachezaji wa muhimu sana katika kikosi chao. Je, wataweza kupindua matokeo leo?

Upande wa pili huku kwa Madrid hakuna shida sana kwani rekodi zinasema kuwa Ajax hajawahi kumfunga Real madrid au kumtoa katika hatua za mtoano katika ligi ya mabingwa Ulaya kwa miongo ya karibuni. Na hata kwa uchezaji wa mechi yao ya kwanza unaweza kuona jinsi AJAX wanavyocheza vizuri lakini wanashindwa kuzitumia nafasi wanazozitengeneza (umaliziaji ni tatizo).

Real Madrid ni wakongwe na magwiji wa hii michuano, siwaoni wakipoteza hii mechi. Ajax wajipange sana kama wanataka kupata matokeo katika mechi hii. 

TUPE UTABIRI WAKO. NANI ANAPITA KATIKA WANAOKUTANA LEO? 

No comments: