LIPUMBA ATOA ONYO KALI KWA WANAOPORA MALI ZA CUF - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

LIPUMBA ATOA ONYO KALI KWA WANAOPORA MALI ZA CUF

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema chama hicho hakitawavumilia wanaopora mali za chama hicho na kuzihamishia Chama cha ACT-Wazalendo.


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam leo Jumanne Machi 19, Profesa Lipumba amesema hatua hiyo ni utapeli na wizi wa wazi, hivyo chama chake kitafuata utaratibu wa kisheria kuzirejesha.

“Hili ni jambo la kisheria, mali za chama zitaendelea kuwa za chama, hao wanaobadili rangi majengo ya chama ninawaambia, akili za Maalim Seif wachanganye na zao, kwa sababu jinai itawahusu wao binafsi na huyu maalim hatakuwa nao,” amesema Profesa Lipumba.

Kumekuwa na picha na video nyingi mtandaoni zikionyesha watu wakibadilisha rangi za ofisi za CUF na kushusha bendela za chama hicho na kupaka rangi za chama cha ACT-Wazalendo.

Vigogo waliotimuliwa CUF 

Licha ya jana Jumatatu Profesa Lipumba kulieleza Mwananchi kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ni miongoni mwa waliofukuzwa kutokana na mwenendo wake wa kukidhoofisha chama hicho pia wamo wengine.
 Leo tena Profesa Lipumba amewataja wanachama wengine ni Ismail Jussa, Mohammed Nur, Issa Kheri,  Salim Biman,na Said Ali Mbarouk  wa Zanzibar. Mbarala Maharagande, Abdallah Katawi na Joran Bashange wa Tanzania bara.
Hata hivyo, baadhi ya wanachama hao waliofukuzwa tayari leo Jumanne wamekabidhiwa kadi za chama cha ACT- Wazalendo akiwamo Maalim Seif.
Loading...

No comments: