LIVERPOOL YAICHAPA SPURS, YARUDI KILELENI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 31, 2019

LIVERPOOL YAICHAPA SPURS, YARUDI KILELENI

Liverpool imerudi kileleni mwa Ligi Kuu England kwa kishindo baada ya kuichapa Tottenham Spurs kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Anfield.


Mabao ya Liverpool yalifungwa na Roberto Firmino katika dakika 16 pamoja na lile kujifunga kwa beki wa Spur, Toby Alderweireld katika dakika 90, wakati Lucas Moura akifunga bao la kufutia machozi kwa wageni dakika 70.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kuongoza ligi kwa pointi 79, wakati mabingwa watetezi Manchester City wakishuka nafasi ya pili na pointi zao 77, huku Spurs ikibaki na pointi zake 61 sawa na Manchester United katika nafasi ya tatu na nne.

Bao la kujifunga Alderweireld limerudisha matumaini ya Liverpool ya kupata ubingwa wa kwanza baada ya kusubiri kwa miaka 30.
Loading...

No comments: