Maalim Seif hajahama Chama, amefukuzwa - Prof. Lipumba - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

Maalim Seif hajahama Chama, amefukuzwa - Prof. LipumbaMwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahi Lipumba amewataka Wanachama wa chama hicho wanaotaka kukihama chama na kuhamia ACT Wazalendo kuungana na katibu mkuu wa Zamani Maalim Seif Shariff Hamadi, kuchanganya akili zao na kutokurupuka kwani wanaweza kujulikuta wamekuwa bendera fuata upepo pasipo kujua upepo una uelekeo gani.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Dar es Salaam, Prof. Lipumba amesema kuwa kwanza kabla ya Maalim Seif kukihama chama hicho tayari alikuwa amefukuzwa."Mimi na sisi kama Chama cha Wananchi CUF tunachokijua Maalim Seif alifukuzwa kuwa mwanachama wa chama chetu kwenye mkutano mkuu uliopita, baada ya kubaini hana nia njema ya chama na anataka kukidhoofisha sio kwamba amehama chama bali amefukuzwa," amesema Prof. Lipumba.

Utakumbuka hapo jana  Marchi 18, 2018 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif  alitangaza kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo. Hiyo ni baada ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kutimua kiongozi hiyo.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG HAPA  blog  Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...

No comments: