MAJERUHI YAWAANDAMA MADRID: CARVAJAL NJE KWA WIKI 4, VINICIUS NJE KWA WIKI 8 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

MAJERUHI YAWAANDAMA MADRID: CARVAJAL NJE KWA WIKI 4, VINICIUS NJE KWA WIKI 8


Majeruhi yameanza kuwaandama klabu ya Real Madrid hasa baada ya kuwapoteza wachezaji wake wawili muhimu katika kikosi hicho ndani ya wiki hii tu. 
Beki Daniel Carvajal atakuwa nje ya uwanja kwa wiki zisizopungua 4 akiuguza majeraha ya paja aliyoyapata katika mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Ajax ambapo Madrid walifungwa 4-1 na kutilewa katika mashindano hayo. 

Ukiachana na beki huyo, mwingine ambaye naye aliumia siku hiyo ni winga wa kushoto, mbrazil Vinicius Jr ambaye amekuwa katika kiwango kizuri mno tokea awe anaanzishwa katika kikosi cha kwanza na kocha Santiago Solari. 


Vinicius atakuwa nje kwa miezi 2 (wiki 8) kutokana na majeraha ya goti na Real Madrid wanabidi watafute mbadala wa wachezaji hawa wawili haraka iwezekanavyo ili kuweza kushinda japo mechi chache zilizobakia msimu huu. 

Loading...

No comments: