MAKALA: ZIFAHAMU SHERIA ZA KODI YA MAPATO SEHEMU YA KWANZA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 7, 2019

MAKALA: ZIFAHAMU SHERIA ZA KODI YA MAPATO SEHEMU YA KWANZA


UTANGULIZI:
Makala hii inahusu masuala ya kodi kwa wanaoanza biashara lakini vilevile itagusa sheria na biashara kwa ujumla wake. lengo ni kuzidi kuelimishana kwa wasiofahamu na vilevile kukumbushana kwa wenye ufahamu na kuongezeana elimu kwa michango mbalimbali itakayoletwa kutoka kwa wanajukwaa.

BIASHARA NA AINA ZAKE: 
Biashara ni kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalmu, wito na makubaliano ya kipekee yenye nia ya kupata faida kwa kifupi ili nisiwachoshe. 

Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, biashara zimegawanyika katika makundi manne:

1. Biashara ndogo sana;
Ina idadi ya waajiriwa kuanzia mmoja hadi wanne, na Mtaji wake ni kuanzia Tsh milioni 1 hadi 5

2. Biashara ndogo
Ina idadi ya waajiriwa 5 hadi 49, na mtaji wake ni kuanzia milioni 5 hadi milioni 200

3. Biashara za kati
Ina idadi ya waajiriwa 50 hadi 99 na mtaji ni kati ya milioni 200 hadi milioni 800

4. Biashara Kubwa
Ina idadi ya waajiriwa zaidi ya 100 na mtaji zaidi ya milioni 800.

Vigezo vingine vinavyotumika na Mamlaka ya Mapato kuweka madaraja ya walipa kodi ni kulingana na kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka. 

SHERIA ZA KODI: 
Shera hizi zinamgusa anaeanza biashara

1. Sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004
2. sheria ya kodi ya Ongezeko la thmani (VAT) ya mwaka 2014 kwa anefuzu kusajiliwa
3. Sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972
4. sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015

Sheria hizi zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia kodi za ndani

A: Sheria ya Kodi ya Mapato
Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapto yake yanatokana na vyanzo mbalimbali km vilivyoainishwa ktk sheria kama vile
a) Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika
b) Ajira yoyote afanyayo mtu
c) Uwekezaji ktk rasilimali. Mfano nyumba, ardhi na hisa
d) Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio "Final Withholding Tax. Mf: Kodi ya malipo ya pango, malipo ya gawio kutoka ktk kampuni kwa Mtz, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (mrahaba)

B: Mapato yatokanayo na biashara
kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 ikarejewa mwaka 2006, Mapato yanayotozwa kodi kutokana na biashara ni Faida au Ziada itokanayo na biashara kwa mwaka wa mapato. Mapato hayo ni pamoja na:
1. Faida kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma za biashara
2. Malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya au kutofanya biashara kulingana na makubaliano ya upande wa pili
3. Zawadi au Takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara
4. Kiasi cha mapatoyanayohusiana na biashara ambayo vinginevo yangekuwa mapato ya uwekezaji ktk rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba`

C: Taratibu za kufuatwa na mtu anaeanza biashara kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) pamoja na malipo ya kodi na mengineyo:
Mtu anaeanza biashara atatakiwa kuomba TIN kutoka TRA ambapo vielelezo hv vitahitajika
1. Fomu za maombi ya TIN kwa mtu binafsi (zinatolewa TRA)
2. Barua ya utambulisho wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (hutolewa na TRA)
3. Mkataba wa pango kwa aliepanga eneo la biashara au kielelzo cha umiliki wa eneo la biashara kama hati, ofa au karatasi za malipo ya kodi ya majengo
4. Kopi ya kitambulisho cha Taifa, Leseni ya udreva, paspoti ya kusafiria au kitambulisho cha kupigia kura
5. Picha ndogo ya paspoti saizi

Mhusika utaulizwa juu ya biashara yako "business assessment". baada ya hapo utaambiwa kiasi cha kodi utakayostahili kulipa kutokana na mauzo ya biashara unayofanya au unayotarajia kuifanya. baada ya maelezo haya taratibu nyingine zitaendele na hatimaye utapata TIN.

Kwa leo naomba tuishie hapa sehemu ya kwanza kutokana na majukumu. Tutaendelea sehemu ya pili. 
Loading...

No comments: