Marehemu Michael Jackson azidi kuandamwa na kashfa ya unyanyasaji kingono - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

Marehemu Michael Jackson azidi kuandamwa na kashfa ya unyanyasaji kingonoMakumbusho ya watoto ya Indianapolis imetoa vitu vyote vinavyomuhusu Michael Jackson kufuatia documentary ya Leaving Neverland inayofichua vitendo vya unyanyasaji wa kingono vinavyodaiwa kufanywa na msanii huyo kipindi cha uhai wake.

Kwenye makumbusho hayo kulikuwa na Kofia na gloves ambazo Michael Jackson amewahi kuzitumia jukwaani, Pia kulikuwa na Poster kubwa la mfalme huyo wa Pop lakini kwasasa vyote vimeondolewa.

Vijana wawili waliowahi kufanya kazi na Michael Jackson siku za nyuma wamejitokeza na kudai mfalme huyo wa Pop amewahi kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa muda wa miaka mingi waliyofanya kazi na  muimbaji huyo.
Loading...

No comments: