MASHABIKI WA REAL MADRID WAMTUPIA LAWAMA RAISI WAO PEREZ KWA KLABU HIYO KUTOFANYA VIZURI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

MASHABIKI WA REAL MADRID WAMTUPIA LAWAMA RAISI WAO PEREZ KWA KLABU HIYO KUTOFANYA VIZURI


Nchini Hispania mnamo juzi na jana mashabiki wa Real Madrid wamekuwa wakitoa maoni yao kwenye tovuti ya AS.Com kuhusiana na mwenendo wa klabu yao, je wanaridhishwa nao?, nani alaumiwe na kipi kifanyike.  

Katika maoni hayo, mashabiki 71% wanaamini kwamba Florentino Pérez ndio wakutupiwa lawama kutokana na majanga ya klabu, huku 12% wanaamini kwamba wachezaji kikosini ndio wanaoiangusha timu, na 10% imewaangukia makocha Santiago Solari na kocha wao aliyepita Lopetegui. 

Sababu kubwa ya asilimia 71 kumuangukia Perez imetokana na mpango wake wa kubana matumizi kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita ili kuuboresha uwanja wa Bernabeu. Tangu mwaka 2015 Real Madrid wametumia kiasi cha Euro Milioni 359.4 huku Barcelona wakiwekeza kiasi cha Euro Milioni 797.1 kwenye kuboresha kikosi chao. 
Loading...

No comments: