MAUMIVU YA GOTI KUMUWEKA NJE YA UWANJA VINICIUS JR SI CHINI YA WIKI 8.. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 6, 2019

MAUMIVU YA GOTI KUMUWEKA NJE YA UWANJA VINICIUS JR SI CHINI YA WIKI 8..

vinicius

Klabu ya Real Madrid wamethibitisha kwamba mchezaji wao kinda Mbrazil na winga wa kushoto Vinicius Jr ameumia goti lake la kulia kwenye mechi ya jana ya UEFA champions League dhidi ya Ajax. 

Madrid bado hawajaainisha wazi kuwa atakuwa nje ya dimba kwa muda gani lakini Jarida la AS limejaribu kuwasiliana na wataalamu wa majeraha ya goti wameambiwa kwamba jeraha kama hilo huwenda likawemuweka Vinicius Jr nje ya dimba kwa muda wa wiki zisizopungua 8. 

Hili halitokuwa pengo kwa Real Madrid tu bali hata kwa kocha wa timu ya taifa ya Brazil Tite ambaye naye alimuita katika kikosi cha Brazil kwa ajili ya mechi dhidi ya Panama na Czech Republic baadae mwezi huu. 


Loading...

No comments: