MBEGU FEKI ZINASABABISHA HALI YA USALAMA WA CHAKULA KUWA MBAYA BARANI AFRIKA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

MBEGU FEKI ZINASABABISHA HALI YA USALAMA WA CHAKULA KUWA MBAYA BARANI AFRIKA


Katibu Mkuu wa shirikisho la mbegu la kimataifa Bw. Michael Keller, amesema kuingia kwa mbegu feki na zisizo na kiwango barani Afrika, kumefanya hali ya usalama wa chakula katika nchi za Afrika kusini mwa Sahara izidi kuwa mbaya.

Bw. Keller amesema hatua zinatakiwa kuchukuliwa ili kuhakikisha wakulima wadogo wadogo wanapata mbegu bora kwa bei nafuu. Akiongea kwenye mkutano mjini Mombasa, Bw. Keller pia amesema kuna haja ya kupitisha njia ya pamoja ya kuhakikisha kuwa wakulima barani Afrika wanapata mbegu rasmi zinazohimili wadudu, magonjwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakati hayo yanajiri mjini Mombasa imefahamika kuwa wazimbabwe milioni 7 wanakabiliwa na njaa kwa mwaka huu kutokana na ukame, na watahitaji msaada wa chakula. Idadi hiyo ni nusu ya wazimbabwe wote.

CHANZO: SWAHILI CRI 
Loading...

No comments: