Mbowe Afungukia Uamuzi wa Maalim Seif Kwenda ACT-Wazalendo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

Mbowe Afungukia Uamuzi wa Maalim Seif Kwenda ACT-Wazalendo


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nchini, Freeman Mbowe amesema kilichotokea kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo ni sehemu ya mapambano.

“Maalim na timu yake bado ni sehemu muhimu sana katika mapambano haya, tunawatakia kila la kheri,” Mbowe aliliambia na gazeti la Mwananchi muda mfupi baada ya Maalim Seif autangazie umma wa Watanzania kuwa yeye, viongozi na wanachama wa chama hicho wanaomuunga mkono wanahamia ACT- Wazalendo.

 Licha ya kuwatakia maisha mema huko ACT- Wazalendo lakini amewaomba wakafanye siasa kuanzia ngazi za chini ili kuhakikisha malengo ya kuwapigania wananchi yanafikiwa.
Loading...

No comments: