Mikataba yamuweka pabaya msanii Kanye West - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 6, 2019

Mikataba yamuweka pabaya msanii Kanye West
Imefahamika kuwa mikataba aliyosaini msanii Kanye West siku za nyuma inamtaka kufanya kazi maisha yake yote. Kanye ataendelea kutengeneza na kuachia miziki mipya kwa muda mrefu sana.

Mwezi wa kwanza iliripotiwa kuwa Kanye West alifungua mashtaka dhidi ya kampuni ya EMI na Roc-A-Fella Records ili kuvunja mikataba aliyosaini nao siku za nyuma wakati anatoka.

Hata hivyo mtandao wa Hollywood reporter umepata kopi ya nakala za kampuni ya EMI kwenye kesi hiyo ambayo inaonesha kuwa mikataba haimruhusu Kanye kuacha kufanya kazi ya muziki maisha yake yote.

Kwenye mashtaka yake KanyeWest amesema kuwa ameifaidisha kampuni hiyo kwa miaka mingi na anataka apewe haki miliki ya kazi zake ambazo amezitengeneza kuazia Oktoba 2010.

Loading...

No comments: