Mitandao ya Rais Kenyatta yafungiwa


Mitandao ya Rais Kenyatta yafungiwa
Akaunti za mitandao ya kijamii za Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, katika mitandao ya Facebook, na Twitter,  zimefutwa kwenye mitandao leo asubuhi Machi 22, 2019.

Akaunti hizo zimefutwa ikiwa ni muda mfupi, baada ya kutoa ujumbe  ambao ulikuwa unasema kwamba hakuna atakayepona kwenye vita dhidi ya ufisadi.

“Kama wewe ni fisadi tutapigana na wewe. Unaweza ukawa dada yangu, kaka au mtu wa karibu na mimi kwenye siasa. Siwezi kushikamana au kukubaliana na hilo katika jitihada zangu, nitaendelea kuimarisha umoja wa Kenya” Yalisomeka maneno yaliyoandikwa Twitter.


Mkuu wa wafanyakazi wa ofisi ya Rais, Nzioka Waita  amesema kwamba akaunti hizo zimezuiliwa kwa muda.

“Hii ni kutokana na kuingiliwa kiharamu kwa akaunti rasmi za mitandao ya kijamii za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta. Akaunti zote rasmi za mitandao ya kijamii zimesimamishwa kwa muda kwa ajili ya kuruhusu kufanyika marekebisho yanayotakiwa,” amesema Waita. 

Post a Comment

0 Comments