MKHITARYAN KUWEKWA SOKONI ILI IPATIKANE FEDHA YA KUSAJILI WANNE WAPYA NDANI YA ARSENAL.


Kocha wa Arsenal Unai Emery anahitaji takribani wachezaji wanne majira haya ya kiangazi na anajiandaa kumuuza Henrikh Mkhitaryan ili kuondoa mshahara wake mkubwa kwenye vitabu vya uhasibu ndani ya Arsenal. 

Kiungo huyo alihamia Arsenal kwa dili la kubadilishana wachezaji na Man United ambapo Alexis Sanchez alihamia Old Trafford na alipewa mshahara wa Pauni 180,000 na kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa klabuni hapo. 

Arsenal watakuwa na kiasi kidogo cha usajili majira ya kiangazi endapo watashindwa kufuzu kucheza UEFA msimu ujao ikimaanisha kwamba watahitaji kuuza wachezaji ili kutunisha mfuko wao wa usajili.

"The Gunners" hawatopokea ada yoyote kutoka kwa Aaron Ramsey, Peter Cech na Danny Welbeck ambao wanatarajiwa kuondoka wakiwa wachezaji huru, lakini wana matumaini ya kupata wanunuaji wa Mkhitaryan. 

Wachezaji wengine ambao wanaweza kuuzwa ndani ya Arsenal ni pamoja na Mohamed Elneny, Calum Chambers na Shkodran Mustafi. 

Post a Comment

0 Comments