MSIMU WA PILI WA LIGI KUU WANAWAKE (SERENGETI LITE WOMEN'S PREMIER LEAGUE) KUANZA JUMAMOSI MARCH 9, 2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

MSIMU WA PILI WA LIGI KUU WANAWAKE (SERENGETI LITE WOMEN'S PREMIER LEAGUE) KUANZA JUMAMOSI MARCH 9, 2019

Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa wanawake, Amina Karuma akizungumza kuhusu msimu wa pili wa ligi kuu ya Wanawake Tanzana Bara maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League unatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi, Machi 9 2019 huku timu 12 zinatarajia kuchuana vikali kwa mfumo wa nyumbani na ugenini.

Msimu wa pili wa ligi kuu ya Wanawake Tanzana Bara maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League unatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi, Machi 9 2019 huku timu 12 zinatarajia kuchuana vikali kwa mfumo wa nyumbani na ugenini. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa wanawake, Amina Karuma alisema wanatarajia kuona msimu huu unakuwa na ushindani kwa timu zote na hatimaye kupata bingwa anayestahili. 

Karuma amepongeza udhamini wa kinywaji cha Serengeti Lite ambao pamoja na mambo mengine umewezesha kuifanya ligi kuwa na ushindani mkubwa na kuleta mvuto wa aina yake. 

“Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite imeweza kuleta ushindani mkubwa baina ya timu zinazoshiriki na hata ukitazama matokeo unaweza kuona ni jinsi gani ambavyo ligi hii imekuwa na msisimko wa aina yake,” alisema 

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha msimu wa pili unakuwa bora zaidi, imefanyika semina kwa ajili ya viongozi wa klabu na wasimamizi wa michezo wakiwamo marefa ili kuwanoa juu ya namna bora ya uendeshaji wa ligi. 

Kwa upande wake, George Mango, Ofisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa Ligi hiyo kupitia kinywaji cha Serengeti Lite, amesema udhamini huo umelenga kuongeza hamasa na kuleta ushindani wa ligi hiyo ya wanawake. 

Ofisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti wadhamini wakuu wa Ligi ya Wanawake(SWPL) George Mango (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimu wa pili wa Ligi hiyo kupitia kinywaji cha Serengeti Lite,

Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji cha Serengeti Lite imeweza kuwekeza jumla ya Sh450 Milioni kama ufadhili wa ligi hiyo ya wanawake nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kama sehemu ya kuendeleza michezo hususan mpira wa miguu nchini.

Aidha, SBL imekuwa ikitilia mkazo uendelezaji wa michezo nchini hasa katika mpira wa miguu ambao mbali na kupendwa na watu wengi umekuwa chachu katika kuinua vipaji mbalimbali hapa nchini.

 TIMU ZITAKAZOSHIRIKI MSIMU WA PILI WA LIGI KUU YA WANAWAKE (SWPL)

1. KIGOMA SISTERZ- KIGOMA
2. SIMBA QUEENS – DSM
3. ALLIANCE GIRLS –MWANZA
4. BAOBAB QUEENS – DODOMA
5. MLANDIZI QUEENS – PWANI
6. JKT QUEENS – DSM
7. PANAMA – IRINGA
8. EVERGREEN –DSM
9. MARSH ACADEMY – MWANZA
10. MAPINDUZI QUEENS – NJOMBE
11. YANGA PRINCESS –DSM
12. TANZANITE – ARUSHA.

Loading...

No comments: