Mtanzania kutunukiwa tuzo ya mwanamke jasiri dunianiMkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga ametajwa kama miongoni mwa wanawake 10 watakaotunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri Duniani (International Women of Courage Award), 2019, tuzo inayoandaliwa na Ikulu ya Marekani chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Mike Pompeo, Tuzo hilo linatarajiwa kutolewa rasmi kesho.

Kwa mujibu wa taarifa katika tovuti ya Ikulu ya Marekani, Bw. Pompeo atawatunuku tuzo wanawake 10 waliofanya mambo kwa ujasiri/uthubutu zaidi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.
Hafla ya utoaji wa tuzo itafanyika Machi 7, 2019 saa 4:00 Asubuhi Washington DC sawa na saa 12:00 jioni Tanzania na  mgeni wa heshima akiwa ni Mke wa Rais wa Marekani Bi. Melania Trump atakuwa .

Bi. Anna Henga ambaye alitwaa mikoba ya kuongoza LHRC kutoka kwa Dr. Hellen Kijo-Bisimba ametajwa kama moja ya wanawake watakaotunukiwa tuzo hiyo kufuatia juhudi zake katika utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania na. Wanawake wengine tisa watakaotunukiwa tuzo hiyo wanatoka katika mataifa ya Bangladesh, Burma, Djibouti, Egypt, Jordan, Ireland, Montenegro, Peru na Sri Lanka.

Tuzo ya International Women of Courage ilianzishwa mwaka 2007 kutambua mchango wa wanawake wanaojitoa kwa nguvu na ujasiri kama viongozi katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao bila kujali hatari ya maisha yao binafsi.

Post a Comment

0 Comments