MTOTO WA B.I.G NOTORIUS AMUENZI BABA YAKE KWA KUFUNGUA KAMPUNI YA BANGI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 12, 2019

MTOTO WA B.I.G NOTORIUS AMUENZI BABA YAKE KWA KUFUNGUA KAMPUNI YA BANGI


Miaka 22 ya kifo cha The Notorious B.I.G imeadhimishwa juzi March 9, nguli huyo wa Hip Hop alifariki kwa kupigwa risasi mjini Los Angeles ambapo alimiminiwa risasi na 4 kumpata wakati akitokea katika sherehe ya Diddy.

Sasa wakati dunia ikianza kutafuta mrithi wake, mtoto wake C.J. Wallace alionekana kuwa ataendeleza alichokiacha baba yake, kitu ambacho kimekuwa tofauti. Sasa katika kuadhimisha kumbukumbu hiyo ya miaka 22, mwanae amefungua kampuni ya Bangi (cannabis company) akishirikiana na baba yake wa kambo Todd Russaw.

Kampuni hiyo ameipa jina la 'Think BIG' kwenye ukurasa wake wa instagram aliandika "Today I am so proud to announce the launch of Think BIG, my first business!". 

Kibongobongo mnamuelewaje huyu mwana? 
Loading...

No comments: