Mtoto wa Ruge Awaliza Wengi... amuombea msamaha baba yake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 3, 2019

Mtoto wa Ruge Awaliza Wengi... amuombea msamaha baba yake

Mtoto wa Ruge  Awaliza  Wengi... amuombea msamaha baba yake
Familia ya Ruge Mutahaba wamesema wanatambua Ruge aliwahi kuwakosea watu kwa kuwa yeye ni binadamu hajakamalika.

Mtoto mkubwa wa Ruge aitwaye Mwachi  amesema Familia inaomba msamaha kwa niaba yake na imewasamehe wote waliomkosea pia.

“Ninamuombea msamaha baba yangu kwa wale wote aliowakosea enzi za uhai wake, nasi tunawasamehe wote waliomkosea baba,” amesema Mwachi wakati akisoma wasifu wa baba yake

Amesema baba yake alikuwa mtu aliyejitoa kwa wengine mpaka familia ilifikia wakati inaona watu wa nje wanamfaidi kuliko wao.

“Alitenga muda mwingi kusaidia kwa kuzingatia misingi ya utu, alipambana kwa hali zote kufanikisha mambo mengi katika jamii,” alisema huku akijitahidi kujizuia kutoa machozi
Loading...

No comments: