MULLER ASHANGAZWA NA UAMUZI WA JOACHIM LOW KUWAACHA YEYE NA WENZAKE TIMU YA TAIFA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

MULLER ASHANGAZWA NA UAMUZI WA JOACHIM LOW KUWAACHA YEYE NA WENZAKE TIMU YA TAIFA


Mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani, Thomas Muller, ameonyesha kuchukizwa na taarifa iliyotoka wiki hii kuwa yeye pamoja na wenzake wawili (Jerome Boateng, Matts Hummels) hawapo tena kwenye mipango ya kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani na amesema kwamba atapigana mpaka kurejea kwenye kikosi cha kocha Joachim Low. 

"Nilishangazwa na uamuzi wa kocha na ninapozidi kufikiria kuhusu uamuzi huo na jinsi ulivyofanyika , unanipa hasira". 

"Wote wanaonijua mimi wanajua kwamba mimi ni mpiganaji , na kwa hili kichwani kwangu, nataka kusema kuwa Mchezo haujaisha bado". Alimalizia Muller ambaye bado anaona ana nafasi ya kuichezea zaidi timu yake ya taifa. Je lengo lake litafanikiwa? 
Loading...

No comments: