Mwakinyo: Sijaona Bondia wa Kupigana Naye Bongo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 29, 2019

Mwakinyo: Sijaona Bondia wa Kupigana Naye Bongo


Mwakinyo: Sijaona Bondia wa Kupigana Naye Bongo

Mwakinyo: Sijaona Bondia wa Kupigana Naye Bongo

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, amesema kuwa hajaona bondia wa kupigana naye hapa nchini na jeuri hiyo anaipata kutokana na udhamini anaoupata kutoka Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Michezo, SportPesa.

Kauli hiyo, aliitoa  Jumanne ya Machi 26, 2019 mara baada ya kutembelea ofisi za Global Group inayochapisha magazeti ya  Championi, Spoti Xtra, Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi Mchanganyiko, pamoja na vituo vya mtandaoni vya Global TV Online na +255 Global Radio,  Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

Mwakinyo, wikiendi iliyopita alifanikiwa kumpiga mpinzani wake Muargentina, Sergio Gonzalez kwa KO katika raundi ya tano ya pambano hilo lililopigwa nchini Kenya.

 Akizungumza mara baada ya kutembelea kampuni hiyo, Mwakinyo alisema kuwa malengo yake hivi sasa yanafikiria kupigana mapambano ya kimataifa na siyo kitaifa kutokana na kutomuona bondia mwenye uwezo wa kupigana naye.

Bondia, Hassan Mwakinyo (aliyekunja ngumi) akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa
Mwakinyo alisema, kwa kupitia SportPesa hivi sasa ana uhakika wa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku huku akiwa na uhakika wa kula chakula safi. Ana udhamini wa miaka mitatu wa SportPesa.

“Binafsi sijaona bondia yeyote wa kupigana na mimi kwa bondia wa hapa nchini na hilo lipo wazi kutokana na kiwango changu nilichonacho hivi sasa.

“Nafahamu hivi sasa kila bondia anataka kupigana na mimi, lakini niwaambie kwangu sijamuona, kama yupo basi hamna shida ajiandae na uwekwe mkwanja wa kutosha utakaonishawishi kupigana.

“Nitakuwa tayari kupigana popote pale atakapotaka mpinzani wangu, hata kama ni sebuleni kwake,” alisema Mwakinyo. 
Loading...

No comments: