Naamini kabisa tukiwepo nyumbani tutafuzu - Nahodha wa Simba SC, Bocco - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 13, 2019

Naamini kabisa tukiwepo nyumbani tutafuzu - Nahodha wa Simba SC, BoccoNahodha wa Simba SC, John Boko amesema kuwa anaamini kikosi chao kitafanya vizuri katika
mchezo dhidi ya AS Vita kutokea DR Congo.

Bocco ameeleza hayo mara baada ya kurejea kutokea nchini Algeria ambapo walicheza na JS
Saoura na kupoteza Goli 2-0.

“Tunamshukuru Mungu tumefika salama, tuna mchezo mwingine tutacheza na AS Vita, mimi
naamini kabisa kwa morali tuliyonayo na mbinu za kocha tukiwepo nyumbani tutapambana na
tutafuzu,” amesema Nahodha John Bocco.

Simba SC wanahitaji ushindi katika mchezo wao wa mwisho utakaochezwa siku ya jumamosi katika dimba la uwanja wa Taifa Dar es Salaam ili kuweza kucheza robo fainali ya klabu bingwa Afrika.
Loading...

No comments: