NBA: JAMES HARDEN ATUPIA POINT 58 HUKU ROCKETS WAKIWAUA MIAMI HEAT, WARRIORS WAPOTEZA MECHI YA PILI MFULULIZO

Houston Rockets

James Harden alimaliza mchezo wa usiku wa kuamkia leo akiwa na pont 58, na assist 10 na kuiwezesha timu yake ya Houston Rockets kushinda wakitokea nyuma 121-118 dhidi ya Miami Heat. 

Harden ambaye ni mchezaji bora (MVP) wa ligi hiyo kwa msimu uliopita, alisaidiwa na wenzake kama Austin Rivers aliyekuwa na point 17 katika mirusho 7 kati ya 8, pamoja na Chris Paul ambaye alikuwa katika kiwango bora usiku huo pia. 

Upande wa pili, pamoja na Stephen Curry kumaliza na point 33, rebound 8 na assist 6 bado havikuweza kuwasaidia Golden State Warriors kushinda mchezo wao dhidi ya Orlando Magic ambao walikuwa wamoto sana siku ya leo. 

Wadau wengi wamesema kuwa labda kukosekana kwa Kevin Durant kumechangia kwa kiasi kikubwa kwa Warriors kupoteza mchezo wa pili mfululizo leo. Hali kama hii ilitokea mwezi December mwaka jana lakini Warriors walirudi katika ubora wao na hadi sasa wanaongoza msimamo wa kanda ya Magharibi. 


MATOKEO YA MECHI ZOTE:

  • Miami Heat 118-121 Houston Rockets
  • Golden State Warriors 96-103 Orlando Magic
  • Philadelphia 76ers 108-104 Oklahoma City Thunder
  • Utah Jazz 111-104 Denver Nuggets
  • Minnesota Timberwolves 115-122 Indiana Pacers
  • Cleveland Cavaliers 125-118 New York Knicks

Post a Comment

0 Comments