NBA: LOS ANGELES LAKERS WASHINDWA KUFUZU PLAYOFFS KWA MARA YA 6 MFULULIZO


Ni rasmi sasa kuwa timu ya Los Angeles Lakers imeshindwa kufuzu kwenda hatua ya mtoano kwa upande wa magharibi baada ya kupokea kichapo kingine mapema alfajiri ya leo dhidi ya BROOKLYN NETS kwa 11-106. 

Kwa msiofahamu, hii ni mara ya sita mfululizo LAKERS wanashindwa kufuzu kwenda hatua hiyo ya muhimu sana ya kuelekea kubeba ubingwa. Pia inakuwa ni mara ya kwanza kwa LEBRON JAMES kushindwa kufuzu kwenda hatua ya Playoffs. Mara ya mwisho yeye kushindwa ilikuwa mwaka 2005. 

Katika mchezo huo uluojawa na hisia kubwa, mchezaji JOE HARRIS ndiye aliyeibuka nyota wa mchezo huku akifunga point 26, Rebounds 3 na assist 6. 

Post a Comment

0 Comments